Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Habari

CLUB YA WANAFUNZI YA LATRA CCC SINGE SEKONDARI YATEMBELEWA NA BARAZA


Sekretarieti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC), chini ya uongozi wa Katibu Mtendaji, Bw Daud G. Daudi, imefanya ziara katika Shule ya Sekondari Singe, Mkoa wa Manyara wilaya ya Babati, ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa shughuli za Club ya Wanafunzi na kutathmini namna inavyoendelea kutekeleza majukumu yake.

Katika ziara hiyo, Sekretarieti ilikutana na Mwalimu Mlezi wa Club, na kupata taarifa kuhusu mwenendo wa Club, ushiriki wa wanafunzi na shughuli zinazotekelezwa tangu kuanzishwa kwake. Mazungumzo hayo pia yalitoa fursa ya kubaini maeneo yanayohitaji kuimarishwa ili Club iweze kuendelea kuwa jukwaa la kuwajengea wanafunzi uelewa kuhusu masuala ya usafiri.

Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za LATRA CCC kuhakikisha Club za Wanafunzi zinaendelea kuwa hai na zinatoa mchango katika kuwafahamisha vijana kuhusu haki na wajibu wa mtumiaji, usalama wa usafiri na matumizi sahihi ya huduma za usafiri ardhini.