Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Makala

TABIA YA TABIA KATIKA USAFIRI WA UMMA

Na.Costantino Michael Mihambo

Watumiaji wa huduma za usafiri ardhini watakiwa kuacha tabia ya kugombaniana kwenye kupanda magari mjini na badala yake wageukie ustarabu wa kupanda magari kwa kupanga mstari jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko kwenye sekta ya usafiri Nchini.

Leo  Ngowi Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri ardhini (LATRA CCC) amesema kuwa ni wakati muafaka kwa abiria kurejea kwenye ustarabu tubadilike tuache kufikiri kuwa kuingia kwenye vyombo vya usafiri kwa fujo ni tabia ya kawaida.

Ngowi amesema baada ya uhuru kwenye sekta ya usafiri kulikuwa na ustaraabu hasa abiria kupanda magari kwakupanga mstari lakini baada ya miaka ya 1984 tulipoingia kwenye soko huria ndio tukashuhudia ustaarabu ukaanza kuondoka kidogo kidogo na sasa tunashuhudia abiria wanaonakuingia kwenye magari kwa fujo ni jambo la kawaida.

Ameongeza kuwa wamegundua kuwa tabia hii ya kupanda magari kwa fujo imesababishwa na vichocheo vinavyosababisha watu kuanza kupanda magari kwafujo na kusema kuwa baraza limeona ni vizuri sasa kuja na mpango wa kitaifa kuhamasisha jamii kupanda magari kwa kupanga mstari na kwa kuanzia watatoa elimu ya falsafa ya kubadilisha tabia ya tabia katika usafiri ilikuwezesha abiria kuanza kubadilika na kugeukia tabia ya ustarabu wa kuingia kwenye vyombo vya Usafiri kistaarabu.

Aidha amesema katika mpango huo utashirikisha moja kwa moja madereva wenyewe,makondakta,wamiliki wa vyombo vya usafiri abiria, Jeshi la polisi,LATRA pamoja na vyombo vya habari ambapo baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri ardhini(LATRA CCC),wataandaa mjadala wa majadiliano kwa uwazi ilikupata maoni ya makundi yote hayo ya watumiaji jambo litakalochochea mabadiliko hayo ya tabia kuacha kupanda magari kwafujo.

Leo Ngowi alitaja madhara ya watu kupanda magari kwa fujo kama vile watoto kuathirika kisaikolojia,wazee akinamama wajawazito,watu wenye ulemavu na mahitaji maalumu kukosa haki ya kuingia kwenye vyombo vya usafiri, kujeruhika, kuibiwa, kuambukizana magonjwa,kuondoa unadhifu wa mtu na wakati mwingine hata kusababisha udhalilishaji wa utu wa mtu,nakuitaka jamii ikae tayari kupokea mpango huo.