Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Majukumu

MAJUKUMU YA BARAZA

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA Consumer Consultative Council), lipo kwa mujibu wa Kif. Namba 29 cha Sheria namba 3 ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini, (LATRA) ya Mwaka 2019.

Baraza linawajibu wa:

  • Kuwakilisha maslahi ya watumiaji wa huduma za usafiri kwa njia ya Reli, usafiri wa umma kwa njia ya barabara, usafiri wa chini ya ardhi na usafiri kwa njia ya waya, kwa kuwasilisha, kupata maoni na tarifa na kwa kushauriana na Mamlaka, Waziri mwenye dhamana na wadau wa sekta mbalimbali zinazodhibitiwa;
  • Kupokea na kusambaza tarifa na maoni mbalimbali kuhusu masuala yanayowagusa watumiaji wa huduma zinazosimamiwa na LATRA;
  • Kuunda kamati za Watumiaji wa huduma za usafiri wa Sekta zinazodhibitiwa na LATRA  katika Mikoa na Kushauriana nazo;
  • Kushauriana na wadau , Serikali na makundi ya watumiaji kuhusu huduma;
  • Kuunda majukwaa kwenye maeneo ya shule/vyuo/taasisi zenye Watumiaji wa huduma za usafiri wa Sekta zinazodhibitiwa na Kushauriana nazo;
  • Kufanya utafiti juu ya maslahi, haki, wajibu na masuala mengine yanayogusa watumiaji.