Habari
Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) 2025
Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini limeungana na wafanyakazi kote nchini kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi 2025. Tukiwa mstari wa mbele katika kutetea haki, usalama, na ustawi wa watumiaji wa huduma za usafiri ardhini, tunasisitiza umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujao.
Maadhimisho ya kitaifa ya mwaka huu yamefanyika mkoani Singida.
Kauli mbiu ya mwaka huu: 'Uchaguzi Mkuu 2025: Utuletee Viongozi Wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiriki.'