Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Habari

LATRA CCC imeshiriki katika Kongamano la Tatu la Kimataifa la Uchukuzi na Lojistiki


Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) limeshiriki katika Kongamano la Tatu la Kimataifa la Uchukuzi na Lojistiki linaloendelea katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. Kongamano hili limeandaliwa na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na linatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku mbili, kuanzia tarehe 21 hadi 22 Agosti 2025, likibeba kaulimbiu isemayo: “Tumia Mifumo Bunifu na Endelevu kwa Kuimarisha Usalama wa Sekta ya Usafirishaji.”