Historia
Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA Consumer Consultative Council), lipo kwa mujibu wa kifungu namba 29 cha Sheria namba 3 ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini, (LATRA) ya Mwaka 2019. Sheria ya LATRA imefuta iliyokuwa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), ambapo kwa wakati huo, Baraza lilijulikana kama SUMATRA CCC. Sheria hiyo ilianza rasmi kutumika Tarehe 29 Aprili, 2019,baada ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali ( GN.No. 358) la tarehe 26/04/2019.
Baraza ni Chombo cha Watumiaji wa huduma za Usafiri kwa njia ya mabasi ya Mijini (Daladala), Mabasi ya Masafa Marefu ndani na nje ya Nchi, Magari aina ya Taxi, Pikipiki za Magurudumu mawili na Matatu, pamoja na Usafiri wa Reli. Baraza limepewa dhamana ya kuwakilisha na kutetea maslahi na haki za Watumiaji wa huduma za Usafiri Ardhini.