Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Habari

Maadhimisho ya Siku ya mtumiaji Duniani Mkoani Morogoro


Jukwaa la Watumiaji Tanzania (TCF) limeadhimisha Siku ya Mtumiaji Duniani katika Mkoa wa Morogoro. Katika maadhimisho hayo, wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia, watoa huduma wa sekta zinazodhibitiwa nchini, pamoja na waandishi wa habari, walikutana kwa majadiliano juu ya masuala mbalimbali.

Mjadala huo ulisisitiza umuhimu wa kuthamini mchango wa wadau wote katika kulinda haki za watumiaji na kuhakikisha huduma zinakuwa endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Maadhimisho haya yaliendeshwa chini ya kaulimbiu: "Haki na Maisha Endelevu kwa Mtumiaji."