Habari
LATRA CCC KUCHOCHEA USHIRIKI WA VIJANA KATIKA KUTAMBUA HAKI NA WAJIBU WAO KAMA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA USAFIRI ARDHINI
Kwa lengo la kufahamu maendeleo ya Club za Wanafunzi na kuimarisha ushirikiano na shule, Sekretarieti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC), ikiongozwa na Katibu Mtendaji,Bw Daud G. Daudi, imefanya ziara katika Shule ya Sekondari Sigino, Mkoa wa Manyara.
Wakati wa ziara hiyo, Sekretarieti ilifanya mazungumzo na Mlezi wa Club kuhusu hali ya Club, utekelezaji wa shughuli zake na namna wanafunzi wanavyoshiriki katika shughuli zinazohusiana na elimu ya watumiaji wa huduma za usafiri.
Ufuatiliaji huu unalenga kupata picha halisi ya namna Club zinavyoendesha shughuli zake katika mazingira ya shule, pamoja na kuhimiza ushiriki wa wanafunzi katika kujifunza na kutoa elimu kwa wenzao kuhusu masuala muhimu yanayowahusu kama watumiaji wa huduma za usafiri.
LATRA CCC inaendelea kushirikiana na shule katika kuendeleza Club za Wanafunzi na kuhakikisha vijana wanapata maarifa yanayoweza kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi wanapotumia huduma za usafiri.

