Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Habari

SEKRETARIETI YA BARAZA LA LATRA CCC YATEMBELEA CLUB YA WANAFUNZI – SHULE YA MSINGI MNADANI


Sekretarieti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC), ikiongozwa na Katibu Mtendaji,Bw Daud G. Daudi  ilifanya ziara katika Shule ya Msingi Mnadani jijini dodoma kwa lengo la kufuatilia na kujua hali ya uhai wa Club ya Wanafunzi, kutathmini maendeleo yake pamoja na kujua namna Club hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika kuwajengea wanafunzi uelewa kuhusu masuala ya usafiri na haki za mtumiaji.

Katika ziara hiyo, Sekretarieti ya Baraza ilikutana na Mkuu wa Shule pamoja na Mwalimu Mlezi wa Club, ambapo walipata fursa ya kujadili mwenendo wa Club, mafanikio yaliyopatikana, changamoto zinazowakabili pamoja na fursa za kuendeleza shughuli za Club hiyo.

Aidha, wanafunzi wa Shule ya Msingi Mnadani walionesha vipaji vyao kupitia ngonjera, nyimbo na maigizo, yaliyobeba ujumbe unaohusiana na elimu, usalama na matumizi sahihi ya huduma za usafiri. Maonesho hayo yalionesha namna Club za Wanafunzi zinavyoweza kuwa jukwaa la kujifunza, kukuza vipaji na wakati huo huo kuwafikia wanafunzi na jamii kwa ujumbe muhimu wa mtumiaji wa huduma za usafiri.

Ziara hii ni sehemu ya jitihada za Sekretarieti ya Baraza la LATRA CCC za kuhakikisha kuwa Club za Wanafunzi zinaendelea kuwa hai, zinafanya shughuli zilizokusudiwa na zinapata mazingira rafiki ya kukuza uelewa, ubunifu na vipaji vya wanafunzi.