Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Habari

KLABU YA WANAFUNZI SECHELELA YATEMBELEWA NA SEKRETARIETI YA LATRA CCC; ZAWADI NA ELIMU ZATOLEWA


Sekretarieti ya LATRA CCC, chini ya uongozi wa Katibu Mtendaji Bw Daud G. Daudi, imefanya ziara katika Shule ya Sekondari Sechelela kwa lengo mahususi la kushuhudia maendeleo ya klabu ya wanafunzi shuleni hapo. Mwalimu Mkuu na Walimu Walezi walionyesha ushirikiano wa dhati kufanikisha ziara hii. Wanafunzi walionyesha uelewa mpana kupitia ngonjera zenye ujumbe mzito na maigizo ya kiwango cha juu kuhusu usafiri salama. Baraza lilivutiwa sana na maendeleo hayo na kufanikiwa kutoa zawadi mbalimbali pamoja na vipeperushi vya miongozo ya usafiri ili kuwawezesha wanafunzi hao kuwa mabalozi bora wa LATRA CCC.