Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Habari

Uzinduzi wa Jukwaa la Wafunzi Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini


Wanavyuo nchini wameshauliwa kutumia vyema elimu yao katika kutatua changamoto inayoikabili jamii ikiwemo kuongeza ubunifu katika Sekta Usafirishaji ili kuhakikisha jamii inanufaika na elimu yao.

Ushauri huo umetolewa leo na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka Uthibiti Usafiri Ardhini, (LATRA) Bw.Henry Bantu wakati wa Uzinduzi wa jukwaa la Uniforum katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Amesema wanafunzi ni miongoni mwa wadau muhimu wa kutoa elimu juu ya sekta ya usafiri na usalama barabarani hivyo kupitia wanavyuo elimu itawafikia wananchi kwa ukubwa zaidi.

“Kupitia wanafunzi kunaweza kusaidia kupaza sauti kwa wengine wakafahamu umuhimu wa kuzingatia sheria za barabarani ili kuweza kupunguza ajari za mara kwa mara”. Amesema Bw.Bantu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri Watumiaji Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) Dkt.George Makuke amesema wanampango wa kufikia vyuo vyote vilivyopo nchini ambapo mpaka sasa wameshwafikia wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari na sasa wameanza na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadae kufikia vyuo vingine.

“Tumeanza UDSM nadhani tutafanya vyuo vingine kama sio vitatu au vinne katika mwaka huu 2021 lengo  letu kuhakikisha wanafahamu suala la usalama barabarani na wao kuwa mabalozi wazuri kwa wengine”. Amesema Dkt.Makuke.

Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri Watumiaji Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC ) Bw.Leo Ngowi, amesema kuwa lengo la uzinduzi jukwaa hilo kuhakikisha wanawapa fursa wanafuzi pale wanapopata changamoto au maoni ili waweze kufikisha katika baraza kupitia wanavyuo.

Hata hivyo kwa upande wake Mwenyekiti Mhasisi wa Jukwaa la wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Unforum) Bw.Faizak Musa amesema wao kama wanafunzi ni wadau wakubwa wa vyombo vya usafiri kwahiyo kuwepo kwa jukwaa hilo kutawapa fursa za kutoa maoni na ushauri kwa Serikali kuhusu utoaji huduma za usafiri.