Habari
SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI 2026
Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo, tarehe 1 Mei 2026, limeshiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kimkoa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja yakiwa na Kaulimbiu :
“Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.”
Katika hotuba yake kwa wafanyakazi, Mhe. Chalamila amesisitiza umuhimu wa uwajibikaji, nidhamu ya kazi na ushirikiano katika kuimarisha uchumi wa mkoa na ustawi wa wafanyakazi wote.
Baraza linaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha huduma za usafiri zinakuwa salama, bora na zenye kuzingatia haki za watumiaji na wafanyakazi kwa ujumla.

