Habari
KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTUMIAJI DUNIANI 2026
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Dkt. Balozi Batilda Burian katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mtumiaji Duniani, yaliyoandaliwa na Jukwaa la Watumiaji Tanzania, Tanzania Consumer Forum (TCF) ambapo LATRA CCC ni moja wa mabaraza yanayounda Jukwaa hilo.
Maadhimisho ya hayo hufanyika kila mwaka tarehe 15 Machi, ambapo kitaifa mwaka huu yamefanyika Jijini Tanga, yakiwa na kaulimbiu isemayo "Bidhaa Salama, Watumiaji Wenye Kujiamini."
Mhe. Burian amesisitiza TCF, watoa huduma, mamlaka za udhibiti, na watumiaji kote nchini (Wananchi wote) kuzingatia usalama katika kusimamia, kutoa, na kutumia huduma hapa nchini.

