Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Habari

LATRA CCC KUENDELEA KUSHIRIKI MAONYESHO YA 50 YA BIASHARA YA KIMATAIFA DAR ES SALAAM (SABASABA 2026)


Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) linayo furaha kuwakaribisha wananchi na wadau wote katika Maonyesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), maarufu kama Sabasaba, yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mwaka huu ni wa kipekee sana kwani maonyesho haya yanatimiza miaka 50 (Jubilei ya Dhahabu) tangu kuanzishwa kwake. Katika kuadhimisha hatua hii kubwa, LATRA CCC inaendelea na dhamira yake ya kutoa elimu, kupokea maoni, na kulinda maslahi ya watumiaji wote wa usafiri ardhini nchini.