Habari
NENO LA SHUKRANI-WASHIRIKI WA MAONYESHO YA 46 YA SABASABA 2022
Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri ardhini (LATRA CCC),limewashukuru wadau wote waliotembelea banda la baraza kwenye maonyesho ya kibiashara ya Mwalimu Julius Kambarage (Sabasaba).
Leo Ngowi Kaimu Katibu Mtendaji LATRA CCC amesema kuwa kwenye maonesho hayo baraza lilijipanga kwenye utoaji elimu kwa mtumiaji wa huduma za usafiri ardhini,kutambua haki na wajibu wake,umuhimu wa ukataji tiketi kwa njia ya mtandao na elimu ya kulitambua baraza.
Ngowi amesema kwenye maoneso hayo baraza limefanikiwa kuwafikia zaidi ya wananchi miatano ambao kwa upande wao walishukuru jitihada za baraza kushiriki kwenye maonesho ya sabasaba kwani kwa kufanya hivyo washiriki mbalimbali walifikiwa na kupata nafasi ya kuuliza maswali na kujibiwa na maafisa wa baraza.
Aidha amesema kuwa barza litaendelea kushiriki kwenye maonesho mbalimbali,kutumia mitandao ya kijamii,vyombo vya Habari na kuendesha semina kwa makundi maalumu lengo ni kujenga uelewa kwa watumiaji.
Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza amewataka watumiaji wa huduma za usafiri ardhini kulitumia baraza kutoa changamoto zinazowakabili kwani ndio chombo pekee kilichopewa dhamana kwa mujibu wa sheria kulinda maslahi yao ili kuleta mabadiliko kwenye sekta ya usafiri wa ardhini Nchini.