Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Habari

NAFASI YA MTUMIAJI KWENYE TEKNOLOJIA KATIKA SEKTA YA USAFIRI NCHINI


Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri ardhini lapigia Chapuo matumizi ya teknolojia katika sekta ya usafiri kwani imekuwa mkombozi mkubwa kwa watumiaji wa huduma hiyo Nchini.

Akizungumza kwenye kipindi cha Morning Jam kinachorushwa na kituo cha matangazo Capital radio na Capital Tv,hivi karibuni Kaimu Katibu Mtendaji wa Latra CCC Leo Ngowi amesema watumiaji wanaendelea kufahamu haki na wajibu wao watumiapo vyombo vya usafiri ambapo ni wajibu wa abiria kupaza sauti pindi anapokutana na changamoto mbalimbali kwa kuwa sasa hivi kuna mazingira rafiki yaliyoandaliwa zinazomwezesha abiria kutoa taarifa ikiwemo kuchakatwa na kufanyiwa kazi kwa uharaka zaidi tofauti na miaka ya nyuma.

''Kulingana na kuwepo kwa taratibu za usafirishaji kwenye vyombo vya usafiri abiria anapokuwa kwenye chombo cha usafiri anahaki ya kuwa salama na tunapoongelea haki ya usalama tunamaanisha abiria inapaswa aangalie  mkanda kwenye kiti chake kama unafanya kazi maana tafiti nyingi zinaonyesha,ikitokea ajali abiria aliefunga mkanda kunauwezekano mkubwa kuwa salama tofauti na yule ambae hakuwa amefunga mkanda''alisema Ngowi.

Ngowi ameongeza kuwa abiria akigundua mkanda wa kwenye basi haufanyi kazi ni wajibu wa kutoa taarifa kwa kondakta wa basi husika na taasisi za serikali kama vile latra na jeshi la polisi ambao wanakuwepo kwenye vituo vya mabasi ili hatua nyingine za kisheria zichukuliwe.

''Abiria anahaki ya kuwa salama anapoona gari linakwenda mwendo kasi kinyume na miongozo iliyopo na asisite kutoa taarifa haraka kwa vyombo husika na jambo lingine ni haki ya kupata taarifa ambapo abiria anapaswa kupata taarifa juu ya umuhimu wa kujiandaa mapema kabla ya kuanza safari ni muhimu kupata taarifa juu ya chombo anachotaka kusafiria kwakuwa sheria inamlinda abiria ambae amekata tiketi mtandao kwa muda mrefu na kama akitaka kusitisha safari yake siku moja kabla ya safari sheria inamlinda na anatakiwa kurudishiwa nauli yake yote na kama akichelewa kusitisha safari chini ya saa kumi na mbili atatakiwa kurudishiwa kiwango cha nauli kilichokatwa asilimia kumi na tano tasfiri yake abiria atarudishiwa kiwango cha nauli asilimia themanini na tano na ikitokea anataka kusogeza mbele safari yake basi sheria pia inamlinda abiria huyo hivyo mambo yote haya abiria anapaswa kuelimishwa na baraza tumejipanga vilivyo kutoa elimu katika msimu huu wa kuelekea mwisho wa mwaka.''Alisema Ngowi.

Aliongeza pia kwa kusema kuwa haki ya kusafiri abiria inabidi aangalie nyenzo muhimu zitakazomsaidia na hapa ndio maana baraza  linasisitiza matumizi ya kutumiwa teknolojia katika sekta ya usafiri ambayo imeboresha sekta ya usafiri kwa kiasi kikubwa.

''Utakumbuka ndugu mtangazaji miaka ya nyuma abiria akitaka kusafiri inalazimu afunge safari kutoka nyumbani hadi kwenye kituo cha basi kukata tiketi kisha kurejea nyumbani kujiandaa na safari hapo utaona muda unaopotea kwenda na kurudi,nauli,usumbufu hasa imekuwa changamoto kubwa kwa watu wenye ulemavu lakini kwa sasa abiria anatimiza haki ya kuchagua kwakuwa anawezeshwa kukata tiketi kwa njia ya mtandao na hapa nipongeze Latra pamoja na kituo cha NIDC kwa kazi kubwa waliyofanya kuhakikisha abiria anapata mahitaji ya kukata tiketi pale pale alipo hakuna sababu ya kuhangaika tena''.Alisema Ngowi.

Aidha ameongeza kuwa tukizungumzia teknolojia katika usafiri wa barabara tunaangalia mabadiliko makubwa kwakuwa baraza linasisitiza abiria kuandika jina sahihi ili ikitokea dharura yoyote ikiwemo kupotelewa na mzigo inakuwa rahisi kuupata na inatuwezesha pia kuwa na takwimu sahihi za usafiri Nchini.

Lakini pia teknolojia inamwezesha msafirishaji kuwa na orodha sahihi ya abiria kwenye gari husika kwakuwa tiketi mtandao inamtengenezea mmiliki orodha moja kwa moja hana haja ya kuandaa kwa mkono kama ilivyokuwa inafanyika zamani.

Mwisho kabisa alisema baraza limejitahidi kusogeza huduma karibu na mtumiaji kwakuongeza kamati za watumiaji katika mikoa mbalimbali lakini pia limeimarisha njia za mawasiliano na sasa mtumiaji anaweza kupata  elimu kupitia tovuti ambayo ni latra ccc,mitandao ya kijamii Twitter,Facebook,YouTube,Instagram na barua pepe barua@latraccc.go.tz na kuwataka watumiaji kuendelea kulitumia baraza lao kwao ndio chombo kilichoanzishwa kwa mujibu wa sheria kulinda maslahi ya mtumiaji.