Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Habari

LETENI MAONI NA CHANGAMOTO MBALIMBALI TUTAZIFANYIA KAZI.


Kaimu Katibu Mtendaji LATRA CCC, Leo Ngowi amewakaribisha wadau wote wa Sekta ya usafiri ardhini kutembelea Banda la Jakaya Kikwete Chumba Namba 44, ambapo watapatiwa elimu juu ya haki na wajibu wa mtumiaji na matumizi ya tiketi mtandao.

Akizungumza kwenye akiwa kwenye banda la LATRA CCC, amesema wamejipanga vizuri kuhudumia wadau na kikubwa zaidi katika maonesho ya mwaka huu pia wamekuja na vitabu maalumu vya maandishi nukta nundu kwa ajili ya watu wasiiona wakiwa ni wadau muhimu kwa Baraza.

Kuhusu kuendelea kutoa elimu kwa watumiaji amesema, baraza limekuwa likishiriki maonesho mbalimbali kwakuwa kwa kufanya hivyo, wanakutana na wadau ana kwa ana na kutoa elimu ikiwemo kusikiliza maoni yao na changamoto wanazokutana nazo wakiwa wanatumia huduma za usafiri ardhini."Baraza pia katika kutambua mabadiliko ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano tunatumia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwafikia watumiaji kama vile tovuti www.latraccc.go.tz, Facebook, Instagram, Twitter, YouTube zote zikipatikana kwa Jina la latraccc.