Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Habari

TOVUTI YA LATRA CCC YAZINDULIWA


Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri ardhini (LATRA CCC) limedhamiria kuondoa kero za wasafiri wa Ardhini kwa kutoa elimu katika maeneo mbalimbali  itakayosaidia kuondokana na kero ambazo si za lazima.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Mwita Waitara wakati akizindua Tovuti ya Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri ardhini (LATRA CCC),Oktoba 01 2021 ambayo ni www.latraccc.go.tz.

Amesema kuwa Baraza hilo tayari limeshaanza kutoa elimu ya kuwa wastaarabu wanapotumia vyombo vya moto kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwani visa vya wananchi kutumia madirisha kuingia kwenye vyombo vya usafiri zimepungua.

Hata hivyo Baraza hilo limesema kuwa Wananchi wameanza kuelekezwa kupanda mstari wanapoingia kwenye usafiri ili kupunguza baadhi ya kero zinazozuilika bila gharama yeyote.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la LATRA CCC,Bw.Leo Ngowi amesema kuwa baraza la LATRA CCC linampango wa kuahamisha jamii kuingia kwenye vyombo vya usafiri kwa atakayekuwa wakwanza kufikia kituoni ndiye atakayekuwa wakwanza kupata huduma ya usafiri kistaarabu.

Hata hivyo amesema kuwa watoto, wajawazito, wazee na wagonjwa watapata huduma stahiki na kwa wakati.

Licha ya hayo Bw.Ngowi amesema kuwa wanataka kujenga jamii ambayo itakuwa na ustaarabu katika kutumia huduma ya usafiri hapa nchini pamoja na kuponya majeraha ya muda mrefu kwa abiria kwa kukaa muda mrefu vituoni.

Hivyo baraza la LATRA CCC limedhamiria kuepusha ajali na majeraha ya mwili kwa watumiaji wa usafiri wa aridhini pamoja na kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya kuambukiza.

Ngowi amesema kuwa licha ya kutoa elimu katika jamii kuwa ya kistaarabu lazima jamii iongeze utu, Umoja, upendo na Mshikamano ili kila mmoja aweze kutumia usafiri wa ardhini bila kuwa na kinyongo.

Amesema kuwa baraza la LATRA CCC wanaihimiza jamii kuanza kutumia kieletroniki katika sekta ya usafirishaji kama kutumia E-tiket kwa mabasi ya mijini na masafa marefu ili kuondoa kadhia ya wapiga debe.

Amesema watakusanya maoni kwa jamii juu ya mikinzano inayojitokeza katika sekta ya usafirishaji hapa nchini hasa kwa upande unaomwathiri mtumia huduma ya usafirishaji.