Habari
LATRA CCC YATATHMINI MAENDELEO YA KLABU YA WANAFUNZI GENERAL MSUGURI, YALETA ZAWADI NA VIPEPERUSHI
Katibu Mtendaji wa LATRA CCC Bw, Daud G. Daudi akiongozana na Sekretarieti ya Baraza, ametembelea Shule ya Msingi General Msuguri kwa lengo la kujionea maendeleo ya wanafunzi katika klabu yao ya usalama barabarani. Ugeni huo ulipokelewa kwa ushirikiano mkubwa na Mwalimu Mkuu pamoja na Walimu Walezi wa Klabu. Wanafunzi walionyesha maendeleo makubwa kwa kuwasilisha nyimbo nzuri na maigizo kuhusu haki zao barabarani. Katika kuunga mkono jitihada hizo, Baraza lilitoa zawadi maalum na kugawa vipeperushi vya elimu kwa wanafunzi wa klabu hiyo ili kuongeza hamasa ya kujifunza.

