Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) likiongozwa na Katibu Mtendaji Bw. Daud G. Daudi ,limehudhuria katika kikao cha kupokea maoni ya wadau wa usafiri
wa ardhini kuhusu maboresho ya Sheria Mbili na Kanuni tano za Leseni za Usafirishaji. Kikao hicho kimefanyika Juni 5, 2024, katika Ukumbi wa mikutano Arnautoglou, Dar es Salaam na kufunguliwa wa Bw. Andrew Magombana, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Usafiri kwa njia ya Barabara kutoka Wizara ya Uchukuzi aliyemuwakilisha Prof. Godius Kahyarara, Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi.