Karibu
KARIBU LATRA CCC
Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA Consumer Consultative Council), lipo kwa mujibu wa kifungu namba 29 cha Sheria namba 3 ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini, (LATRA) ya Mwaka 2019. Sheria ya LATRA imefuta iliyokuwa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), ambapo kwa wakati huo, Baraza lilijulikana kama SUMATRA CCC. Sheria hiyo ilianza rasmi kutumika Tarehe 29 Aprili, 2019,baada ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali ( GN.No. 358) la tarehe 26/04/2019.
Baraza ni Chombo cha Watumiaji wa huduma za Usafiri kwa njia ya mabasi ya Mijini (Daladala), Mabasi ya Masafa Marefu ndani na nje ya Nchi, Magari aina ya Taxi, Pikipiki za Magurudumu mawili na Matatu, pamoja na Usafiri wa Reli. Baraza limepewa dhamana ya kuwakilisha na kutetea maslahi na haki za Watumiaji wa huduma za Usafiri Ardhini.
Mpango mpana kwa Mwaka wa Fedha 2021/22 ni kuhamasisha Jamii (Abiria) kuingia kwenye Mabasi kiustaarabu (kwa mstari). Abiria wa kwanza kufika kwenye kituo, kuwa wakwanza kupata Huduma ya Usafiri kiustaarabu. Hii ni kuwawezesha watoto, wazee, akinamama wajawazito, wagonjwa na abiria wote kupata Huduma stahiki, kwa wakati. Kauli mbiu yetu, LATRA CCC SAUTI YA JAMII, INGIA KWENYE BASI KIUSTAARABU.
Ili kuleta tija ya maendeleo katika Sekta ya Usafiri, Baraza linawakaribisha wadau wote, kuwasilisha kero, mapendekezo, au maoni mbalimbali yatakayosaidia kukua kwa Sekta hii. Njia ya kuweza kuwasiliaana nasi ni pamoja na kupitia tovuti hii, Emails: barua@latraccc.go.tz, Instagram: latra_ccc, facebook: latraccc, Twitter: latraccc, Youtube: latraccc
KARIBUNI SANA.