Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Habari

Utaratibu Mpya wa Kupanda Mabasi Waja


Watumiaji wa huduma za usafiri ardhini watakiwa kuacha tabia ya kugombaniana kwenye kupanda magari mjini na badala yake wageukie ustarabu wa kupanda magari kwa kupanga mstari jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko kwenye sekta ya usafiri Nchini.

Hayo yamesemwa na  Leo  Ngowi  Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri ardhini (LATRA CCC) wakati akizungumza katika kipindi cha MorningJam kinachorushwa na Capitalradio ambapo alisema kuwa ni wakati muafaka  kwa abiria kurejea kwenye ustarabu tubadilike tuache kufikiri kuwa kuingia kwenye vyombo vya usafiri kwa fujo ni tabia ya kawaida.

Ngowi amesema baada ya uhuru kwenye sekta ya usafiri kulikuwa na ustaraabu hasa abiria kupanda magari kwa kupanga mstari lakini baada ya miaka ya 1984 tulipoingia kwenye soko huria ndio tukashuhudia ustaarabu ukaanza kuondoka kidogo kidogo na sasa tunashuhudia abiria wanaona kuingia kwenye magari kwa fujo ni jambo la kawaida.

Ameongeza kuwa wamegundua kuwa tabia hii ya kupanda magari kwa fujo imesababishwa na vichocheo vinavyosababisha watu kuanza kupanda magari kwa fujo na kusema kuwa baraza limeona ni vizuri sasa kuja na mpango wa kitaifa kuhamasisha jamii kupanda magari kwa kupanga mstari na kwakuanzia watatoa elimu ya kubadilisha tabia ya tabia katika usafiri ili kuwezesha abiria kuanza kubadilika na kugeukia ustarabu wa kuingia kwenye vyombo vya usafiri.

Aidha amesema katika mpango huo utashirikisha moja kwa moja madereva wenyewe,makondakta,wamiliki wa vyombo vya usafiri abiria,jeshi la polisi,LATRA pamoja na vyombo vya habari ambapo baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri ardhini(LATRA CCC),wataandaa mjadala wa majadiliano kwa uwazi ili kupata maoni ya makundi yote hayo ya watumiaji jambo litakalo chochea mabadiliko hayo ya tabia kuacha kupanda magari kwa fujo.

Leo  Ngowi alitaja madhara ya watu kupanda magari kwa fujo kama vile watoto kuathirika kisaikolojia,wazee akinamama wajawazito,watu wenye ulemavu na mahitaji maalumu kukosa haki ya kuingia kwenye vyombo vya usafiri,kujeruhika,kuibiwa,kuambukizana magonjwa,kuondoa unadhifu wa mtu na wakati mwingine hata kusababisha udhalilishaji wa utu wa mtu,na kuitaka jamii ikae tayari kupokea mpango huo.