Habari
Maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa maarufu Sabasaba
Bw. Daud Daudi, Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC), pamoja na Bi. Fatuma Kulita, mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala - LATRA CCC wametembelea Jengo la LATRA lililopo kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Saba Saba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam.
Maonyesho hayo yalianza Juni 28 na yatafika tamati Julai 13, 2024.