Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Habari

MRADI WA TRENI YA MWENDO KASI MKOMBOZI KWA MTUMIAJI


Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri ardhini wamepongeza uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika mradi wa treni ya mwendo kasi kutoka Dar es Salaam hadi Makutopola Dodoma.

Dkt George Makuke Mwenyekiti wa baraza la Latra CCC amesema hayo kwenye ziara iliyofanywa na wajumbe pamoja na Sekretarieti baraza lengo likiwa kujifunza utekelezaji wa mradi huo kuanzia kipande cha Dar es Salaam Kilosa Mkoani Morogoro.

Dkt Makuke amesema kwenye ziara hiyo wamepata fursa ya kujionea utekelezaji wa mradi huo kwa kupita pembezoni mwa reli kuanzia stesheni ya Dar es salaam hadi kilosa na wamepata nafasi ya kushuhudia kwa ukaribu zaidi vituo mbalimbali vya Kwala,Morogoro ikiwemo na kujionea madaraja ya reli na ujenzi wa uzio ili kuzuia muingiliano wa reli na shughuli za kibinadamu.

Kwa upande wake Kaimu katibu mtendaji Latra CCC Leo Ngowi amesema reli hiyo ya mwendo kasi inaviwango vya kimataifa ikilinganishwa na zingine zilizojengwa kwenye baadhi ya nchi jirani,kwasababu inauwezo wa kwenda mwendokasi wa 160 kwa saa.

''Ukiangalia kwenye ubora reli hii inauwezo wa behewa moja kubeba lingine kwa juu na kuhimili uzito wa tani 35 kwenye kila mzigo alisema Ngowi.

Rehabu Mahaja Mhandisi wa Kipande Mkoa wa Pwani akizungumza wakati ujumbe wa Latra CCC ulipofika kwenye handaki lililopo eneo la Kilosa amesema,mahandaki yote yameunganishwa na madaraja marefu ili kuepusha athari za mto Mkondoa ambao umekuwa ikiathiri miundombinu ya reli za zamani mara kwa mara kwa ujenzi huu utasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda miundombinu ya reli isipate madhara hasa kipindi cha msimu wa mvua kubwa.