Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Habari

ELIMU YA HAKI NA WAJIBU WA MTUMIAJI WA HUDUMA ZA USAFIRI ARDHINI KUTOLEWA KATIKA MAONESHO YA SABASABA


Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini linawakaribisha wadau wote katika maonesho ya 47 ya biashara ya kimataifa ya Sabasaba yanayoanza Juni 28, 2023 hadi Julai 13, 2023 ndani ya viwanja vya maonesho ya biashara ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Saalam. Bi Fatuma Kulita,

Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala LATRA CCC, amesema mtumiaji anahaki ya kuelimishwa kwa kutambua hilo Baraza limejipanga kutoa elimu juu ya haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za usafiri ardhini, lakini pia elimu juu ya umuhimu wa kutumia tiketi mtandao kutolewa katika maonesho hayo.

Ameongeza kuwa Baraza litakuwepo katika banda la Jakaya Kikwete chumba namba 44 wadau mbalimbali wanakaribishwa ili kujifunza mambo mengi. Pia Baraza kwa kutambua usawa wa watumiaji wote umeandaa vitabu vya nukta nundu kwa ajili ya wasioona vikielezea kazi za Baraza, haki na wajibu wa mtumiaji pamoja na matumizi ya tiketi mtandao.

Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala LATRA CCC. Bi Fatuma Kulita ametaja haki za mtumiaji wa huduma za usafiri ardhini ikiwemo, haki ya usalama, haki ya kupata mahitaji muhimu, haki ya kupewa taarifa, haki ya kuchagua, haki ya kusikilizwa, haki ya Kulipwa fidia, haki ya kusafiri katika mazingira Salama, haki ya kuelimishwa, haki ya kugomea huduma au bidhaa zisizokidhi viwango.