Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini

Habari

Mkutano wa kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati za Mikoa(RCC's)


Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) likiongozwa na Katibu mtendaji Bw. Daud G Daudi limefanya ufunguzi wa mkutano wa kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati za Mikoa(RCC's) leo tarehe 12/06/2024 katika Ukumbi wa Mbaraka Mwinshehe mkoani Morogoro.
Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Bw. Andrew Magombana,Kaimu Mkurugenzi
Msaidizi wa Usafiri kwa njia ya Barabara kutoka Wizara ya Uchukuzi na utadumu kwa muda wa Siku Mbili.